Diamond Platinumz atangaza habari njema kwa Wakenya saa chache tu baada ya kupewa talaka na mkewe
- Diamond Platinumz yuko kwenye harakati za kuzindua tawi jipya la studio yake maarufu kama 'Wasafi Records' nchini Kenya
-Diamond alitangaza habari hiyo njema kupitia mtandao wake wa kijamii wa Instagram Alhamisi Februari 15 siku moja tu baada ya mkewe Zari Hassan kutangaza kuvunjika kwa ndoa yao
- Hata hivyo,Diamond hajazungumzia habari za kutengana na Zari kufikia sasa
Mwanamuziki kutoka Tanzania na mmiliki wa studio maarufu ya 'Wasafi Records',Diamond Platinumz ametangaza kuzindua tawi jipya la studio hiyo nchini Kenya.
Habari Nyingine:Shabiki amuita mchezaji Michael Olunga ‘tumbili’ baada ya kushindwa

Habari Nyingine:Mwili wangu haujakusudiwa jela - Musalia Mudavadi
Kupitia ujumbe alioandika kwenye ukurasa wake wa Instagram,Diamond alisema kuwa ananuia kukuza talanta za wanamuziki chipuka humu nchini na kuwasaidia kupata umaarufu katika muziki.
"Kama unavyofahamu mwaka huu @wcb_wasafi tunafungua tawi jipya nchini Kenya, maalum kwa ajili ya kuendelea kunyanyua vijana wenzetu wenye vipaji tokea mtaani. Tafadhali nisaidie kuwajuza vijana wote wenye vipaji Kenya," Diamond aliandika Instagram.
Tuma neno ‘NEWS’ kwa 40227 ili kupata habari muhimu pindi zinapochipuka
Wasafi Records ambayo imevuma Tanzania na Afrika Mashariki inawashirikisha wanamuziki kadhaa akiwemo Diamond ambaye ni mwenyeji,Maromboso ambaye alikuwa wa kundi la Ya moto Band,Rich Mavoko,Rayvanny na Harmonize.
Habari hiyo njema ilijiri siku moja tu baada ya mkewe Diamond, Zari Hassan kutangaza kuvunjika kwa ndoa yao kupitia mitandao ya kijamii.
Zari alimtaliki Diamond Jumatano Februari 14 ambayo ilikuwa siku ya kusherehekea mapenzi kwa wale wapendanao kote ulimwenguni.
Habari Nyingine:Wanaume wana haki ya kuoa wanawake wengi – Mchungaji Nairobi

Aidha,Zari alidai kuwa Diamond hajakuwa mwaminifu katika ndoa yao na amekuwa akimkosesha heshima kila mara.
Alidai kuwa aliamua kutengana na Diamond kama mke wala sio kama mzazi kwa watoto wao.
Read; ENGLISH VERSION
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri: mwangi.muraguri@tuko.co.ke
Tazama habari zaidi kutoka TUKO.co.ke
Subscribe to watch new videosChanzo: TUKO.co.ke
ncG1vNJzZmijmajEorTIpaBnrKWgvG%2Bvzmeinmdia4NyhZdmm6KZnaS7pXnPpZitoZ6qurt5wK2Yp5%2BRr65utMCbmKuhXaO3prnAZqKwmV2srqyxzbKYZquRlnqktMCcn55lpKp6o63AnZhmsZFiuLa8xLCYZqyRoa6srYynmGalm5rEpnrHraSl